Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasilino wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapundaakionesha fomu ambayo wa wanafunzi wanaotaka kupatiwa ufadhili wa kusomeshwa kupitia kampuni hiyo chini ya taasisi ya EABL Foundation kwa mwaka 2011 kwa wanahabari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasilino wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari juu ya kuanza mchakato wa kupata wanafunzi ambao SBL itawapa udhamini wa kimasomo katika Vyuo vya elimu ya Juu nchini. Pamoja nae kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa SBL,Nandi Mwiyombela na Meneja Mawasilano ya ndani ya SBL Imani Lwinga.
Mapunda alisema taarifa kuhusu mchakato zitatolewa katika vyombo mbalimbali vya habari ili kuwawezesha waomba kuziona na baadaye kutuma maombi.
Alisema mpango huo wa ufadhili uko wazi kwa wanafunzi watakaopata alama za juu na kwamba unahusisha wanafunzi wa ukanda mzima wa Afrika Mashariki, ambao hawana uwezo wa kifedha kumudu kugharimia masomo yao.Mapunda alizitaja fani ambazo wanafunzi wake watadhaminiwa kuwa ni pamoja na Biashara, Tekinolojia ya Habari, Uhandisi na Sayansi ya VyakulaAlisema ufadhili utakaotolewa kwa atakaofanikiwa, utajumuisha utajumuisha tuisheni, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na mpango wa kazi.
“Kwa mwaka huu wa ufadhili, tunatarajia kusaili wanafunzi 10 na miongoni mwao, wanafunzi wanne watapata ufadhili kamili wa masomo.Tayari tumewekeza kiasi cha Sh140 milioni kwa ajili ya mpango huu hapa Tanzania,” alisema ofisa huyo.Alifafanua kuwa wanaotakiwa kuomba ni wanafunzi ambao tayari wameshapata barua za kujiunga na moja ya vyuo vikuu nchini.
“Kwa mujibu wa Mapunda kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe na cha Dar es Salaam, shahada zitakazohusika ni Biashara, Uhandisi, Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Mawasiliano.Alisema kampuni imelenga kozi hizo kwa sababu zinawiana na shughuli zake za kibiashara jambo ambalo litawapatia unafuu wa kuwafanyia udahili na kuwatumia wakati wa mafunzo kwa vitendo. Alisema waka jana kampuni ilipokea zaidi ya maombi 500 ya nafasi za mafunzo ya vitendo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasilino wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari juu ya kuanza mchakato wa kupata wanafunzi ambao SBL itawapa udhamini wa kimasomo katika Vyuo vya elimu ya Juu nchini. Pamoja nae kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa SBL,Nandi Mwiyombela na Meneja Mawasilano ya ndani ya SBL Imani Lwinga.
Habari Kamili.>>>>>>vvv
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL), imetangaza kuanza kwa mchakato wa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu katika mwaka huu.Mchakato huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mahusiano na Nawasikliano wa SBL, Teddy Mapunda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.Mapunda alisema taarifa kuhusu mchakato zitatolewa katika vyombo mbalimbali vya habari ili kuwawezesha waomba kuziona na baadaye kutuma maombi.
Alisema mpango huo wa ufadhili uko wazi kwa wanafunzi watakaopata alama za juu na kwamba unahusisha wanafunzi wa ukanda mzima wa Afrika Mashariki, ambao hawana uwezo wa kifedha kumudu kugharimia masomo yao.Mapunda alizitaja fani ambazo wanafunzi wake watadhaminiwa kuwa ni pamoja na Biashara, Tekinolojia ya Habari, Uhandisi na Sayansi ya VyakulaAlisema ufadhili utakaotolewa kwa atakaofanikiwa, utajumuisha utajumuisha tuisheni, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na mpango wa kazi.
“Kwa mwaka huu wa ufadhili, tunatarajia kusaili wanafunzi 10 na miongoni mwao, wanafunzi wanne watapata ufadhili kamili wa masomo.Tayari tumewekeza kiasi cha Sh140 milioni kwa ajili ya mpango huu hapa Tanzania,” alisema ofisa huyo.Alifafanua kuwa wanaotakiwa kuomba ni wanafunzi ambao tayari wameshapata barua za kujiunga na moja ya vyuo vikuu nchini.
“Kwa mujibu wa Mapunda kwa Chuo Kikuu cha Mzumbe na cha Dar es Salaam, shahada zitakazohusika ni Biashara, Uhandisi, Sayansi ya Chakula na Teknolojia ya Mawasiliano.Alisema kampuni imelenga kozi hizo kwa sababu zinawiana na shughuli zake za kibiashara jambo ambalo litawapatia unafuu wa kuwafanyia udahili na kuwatumia wakati wa mafunzo kwa vitendo. Alisema waka jana kampuni ilipokea zaidi ya maombi 500 ya nafasi za mafunzo ya vitendo.
0 comments:
Post a Comment