Nafasi Ya Matangazo

September 01, 2011

Mtangazaji wa East African Redio US Anko Denzel Musumba, aliembeba dogo Hudhaifa Shatry akiwa na mzee wa swahilivilla editor, juu ya mpangilio mzima wa kuanda kipindi cha salamu na pongezi, kilichoandaliwa rasmi na Abou Shatry, Mtangazaji wetu wa East African Redio US, Anko Danzel Musumba, pamoja na mzee wa changa moto yetu, Mubelwa Bandio, ndani ya East African Redio US.

Jana ilikuwa ni sikukuu kubwa ya waislamu Duniani kote siku ya Eid El Fitr, kwa furaha ya kuadhimisha siku hii adhimu ya kupongezana, kutoleana salamu na kutakiana kila la kheri katika mfungo mzima wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani, uliomalizika siku ya jumatatu kumkia jumanne ya Aug,30/2011,

Baadhi ya waumini wa Jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community Washington Metropoli  (TAMCO). wanaoishi hapa DVM hawana  budi, kumpongeza ndugu yetu,  mtangazaji wetu wa East African Redio US, Bwana Denzel Musumba kwa kazi nzuri aliyo ifanya jana katika  kipindi cha salamu za kupongezana na kutakiana  edi jeema,  kupitia East Africa radio LIVE siku ya jumanne Aug 30, 2011 mida ya saa 6: PM hadi 10:PM

Mtangaziji wa Redio hiyo Bwana  Denzel Musumba, aliweza kuunganisha waumini wa dini ya kislamu na wasiokuwa waislamu kutoa pongezi zao mbali mbali na kuwatakia sikuku ya jeema ya Eid El Fitr kupitia kwa njia ya mtandao na simu ya East Africa radio USA, ambayo pia unaweza kusikiliza kwa simu ya mkononi redio hiyo kwa njia ya simu, nambari             (347)857-1206       juu ya maada yoyote inayoongelewa LIVE ikitaka kuchangia maoni yako na kuongea na  mtangazaji wetu ndugu, Denzel Musumba  unabofya numbari (1),yeye atakutajia number zako za mwisho ili kukujulisha ndio wewe atakaeongea nawee na kukupa uwanjaa wakutoa maoni yako. kwa mada iliokuwa hewani.

Siku zote sitochoka kusema hivi, Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo na mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ile, hujenga jamii yenye kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha. Pale panapo mahitaji kuhusu jamii yetu kwa jumla. Hii ni kuonyesha amani, maelewana, upendo, na ustahi wajamii yetu hii tuipendayo katika kipindi hiki kigumu kilichotukabili. Chuki ni sumu ya mapenzi
Posted by MROKI On Thursday, September 01, 2011 1 comment

1 comment:

  1. Shukuran kaka tuwe na moyo mmoja kwa sote wana blog ahsante sana kwa upendo wako!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo