Nafasi Ya Matangazo

August 11, 2011

Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwakaribisha washiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, katika Jumba la Vodacom ambalo litatumika katika kipindi chote cha warembo wakiwa kambini. Katikati ni Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga. Warembo hao wameingia katika Jumba hilo Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wadau wa sanaa ya urembo kutoka makampuni mbalimbali wakiwa katika tafrija hiyo ya kuwakaribisha warembo katika jumba la Vodacom.
 Warembo wakiwa katika uso wa mshangaa kwa jinsi mambo makubwa wanayofanyiwa katika kambi ya mwaka.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (katikati) akiwafundisha namna ya kufungua shampeni warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011.
 Walifauli na kufungua mvinyo huo bila kumwaga hata tone...
 Hakika ilikuwa ni furaha kwao wote...
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania, Hashim Lundenga.akimiminiwa kinywaji chake kisicho na kilevi kutoka kwa warembo.
 Adam Mchomvu a.k.a Papa John kutoka Clouds Media Group, akishow malovedove na wanyange wa Vodacom Miss Tanzania 2011.
 TBC walikuwepo kuwajuza watu yapi yanajiri katika mjengo huo na hapa ni Mwandishi wao Angela Msangi akiwa katikati ya Walimbwende.
 Mziki huu bwana vijana hasa warembo kama hawa huupenda sana ni miondoko ya Kwaito.
Ukicheza Kwaito lazima uwe unazunguluka kwa staili na hapa ni moja ya mizunguko hiyo ya kunesa nesa.
Posted by MROKI On Thursday, August 11, 2011 2 comments

2 comments:

  1. Mbona PICHA nyingi umewachukua za kusimama tu mbona hamna za KUKAA.

    Au hawakukaa?

    We Mroki vipi wewe!?!

    ReplyDelete
  2. Kaka kwani Mwamvita ni MJAMZITO?
    Mbona kama kavaa TENITI?

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo