Nafasi Ya Matangazo

August 29, 2011

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akimsikiliza Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kwa Mbunge wake juu ya kitendo cha kubomolewa choo chake na Mwekezaji Raia wa kigeni na kuzungusha uzio uliofikia  upenuni mwa makazi yake. Mbunge huyo alitembelea kitongoji hicho mwishoni mwa wiki kujionea hali halisi ya mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo.
 Makala akiongozwa kuangalia uzio uliowekwa na muwekezaji huyo na kuzua mgogoro wa ardhi wa kugombea mipaka na wanakijiji. Kushoto ni walinzi wa mwekezaji huyo.
 Mbele akakutana na ujumbe huu ikabidi ausome na kucheka.
 Mbunge Makala akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kinyenze (shati jeupe) Endeni Msangi na mmoja wa wajumbe wa kufuatilia mgogoro huo, Said Ahmad.
 Wananchi wakiwa mkutanoni hapo na Mbunge.
 Mkazi wa Kijijini hapo Ally Kidunda akitoa maelezo juu ya ukweli wa mgogogo huo kijijini hapo dhidi ya Mwekezaji huyo raia wa Kigeni.
Afisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari akijibu hoja za wakazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki wanaolalamika juu ya kuvamiwa na  mwekezaji  Raia wa kigeni  kuuziwa eneo kubwa la ardhi  na kumega sehemu ya mashamba yao, kufunga barabara, shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho. Kushoto ni Diwani wa Mlali, Juma Mrangi, Mbunge wa Mvomero, Amos Makala na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera Anthony Karoli.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki katika harakati za kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo , kufuatia mwekezaji  Raia wa kigeni  kuuziwa eneo kubwa la ardhi  na kumega sehemu ya mashamba yao, kufunga barabara, shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho.
Posted by MROKI On Monday, August 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo