Nafasi Ya Matangazo

August 10, 2011

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikaguwa Gwaride lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo jijini Luanda, Angola leo Agosti 19, baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana Agosti 18.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maafikiano yaliyotokana kuhusu itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu udhibiti wa fedha chafu sambamba na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SADC yaliyoafikiwa katika mkutano  wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC  mjini Luanda Angola jana Agosti 18.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Benard Membe na Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Maendeleo zilizopo kusini mwa afrika (SADC), wakiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya hiyo uliomalizika nchini Luanda Angola.
Makamu wa Rais wa Tanzania,  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe,  Mogan Changirai.
Posted by MROKI On Wednesday, August 10, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo