.jpeg)
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thabit Ramadhani akumueleza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa namna moyo unavyofanya kazi alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam..jpeg)
.jpeg)
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idd Kimario akimpima Shinikizo la damu Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam..jpeg)
.jpeg)
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa akitazama mfano wa saani ya makundi ya chakula alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa akipokea zawadi kutoka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.
Fatma Almasi Nyangasa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kutembelea banda la Taasisi hiyo lililopo
katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya Kilwa jijini.
*************
Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam
Wananchi wametakiwa kutumia fursa ya Maonesh ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA) kutembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili kupima afya zao na kutambua mapema vihatarishi vya magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyoambukiza kupitia kampeni ya Jua Namba Zako.Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Fatma Almasi Nyangasa alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho hayo na kuweza kujua namba zake.
Mhe. Fatma alisema JKCI imewaletea wananchi huduma muhimu zinazowawezesha kufanya uchunguzi wa afya, lakini pia kupata elimu ya kujikinga na magonjwa ya moyo.
“Kuna vitu vingi vya faida katika banda hili kuna huduma zote za msingi zinazohusiana na masuala ya moyo, lakini pia huduma nyingine muhimu za afya zinazopatikana kwa urahisi”, alisema Mhe. Fatma
Aidha Mhe. Fatma alisema kampeni ya Jua Namba Zako ni ya muhimu kwa kuwa inawahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara badala ya kusubiri hadi wanapoumwa.
“Mimi tayari nimezijua namba zangu, fika kwenye banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete upime urefu, uzito, shinikizo la damu na vipimo vingine muhimu ili ujue hali yako ya afya”, alisema Mhe. Fatma
Vile vile Mhe. Fatma aliipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kuifanya Taasisi hiyo kuwa miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma za kisasa za matibabu ya moyo.
Mbali na kampeni ya Jua Namba Zako, Mhe. Fatma aliwahamasisha wananchi kuendelea kushiriki katika kampeni ya Kutoa ni Moyo inayolenga kuchangisha fedha za kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo kupata matibabu katika Taasisi hiyo.



.jpeg)
.jpeg)



0 comments:
Post a Comment