Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2011

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa  kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Yonnes Kihiyo katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni  jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kulia) akishikana mikono na motto yatima, Batuli Saidi katika hafla ambayo Airtel ilikanodhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni  jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa  kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Kawe Huruma Group , Hilda Rwebangira  katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni  jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.

Airtel yatoa msaada wa cherehani 10 kwa vikundi vitatu vya watoto Yatima Dar es Saalam.
 Alhamis 4 Agusti 2011, Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imetoa msaada wa vyerehani kumi  kwa vikundi vitatu vya wanawake vinavyolea watoto yatima jijini Dar Es Salaam ili kuviongezea uwezo wa  kulea watoto wanaolelewa katika vituo hivyo.

 Msaada huo umekabidhiwa na meneja huduma za jamii wa  airtel Tunu kavishe  kwa vikundi hivyo. Vikubdi vilivyofaidika na msaada huo ni  kikundi cha  wanawake cha kulea watoto yatima cha Msasani,kikundi cha Huruma cha Kawe pamoja na kile cha kulea watoto yatima cha Kinondoni.

 Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Bi.Kavishe alisema "AIRTEL itaendelea kugawa  misaada kwa vikundi vya wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia jamii katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo inayakabili hususani katika sekta ya elimu".

 Akipokea msaada huo wa mashine za kushonea, mwakilishi wa  kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Prudencia Kibatara alisema  " Msaada huu  utatusaidia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto hawa ambao tunawahudumia katika vituo vyetu. tunachangamoto nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watoto na kipato kidogo cha uendeshaji vikundi hivi, hivyo tunawapongeza sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jamii.

 kupitia cherehani hizi tutaanzisha madarasa ya ushonaji na ada zitakazolipwa zitatumika kusaidia watoto hawa, vilevile chereharani hizi zitatumika kushona vitambaa na mashuka ambayo yataleta pato katika vikundi na tutaweza hata kuendelea kuwasomesha watoto hawa vizuri" aliendelea kusema bi  Bi Kibatara Aidha Afisa mtendaji wa kata ya msasani .. Swai aliiipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa kujitokeza na kusaidia vikundi hivyo na kutoa angalizo kwa walezi wa vikundi hivyo  kutumia msaada huo kwa manufaa ya watoto na si yao binafsi.

 "Jamani wakina mama naomba huruma zetu za dhati ziendelee hakikisheni mnaendelea kutumia msaada huu mlioupata kama nyenzo ya kuendelea kuwatunza na kusaidia watoto hawa na sio kujifaidisha sisi wenyewe" alisema Afisa mtendaji wa Msasani .

 ..Leo Airtel wameonyesha jinsi wanavyojali jamii wanayoihudumia hivyo naomba tuwaunge mkono ili dhamira yao itimie" alimaliza kwa kusema afisa mtendaji...

 Vituo vilivyopa msaada huo viko jijini Dar es salaam ambavyo kwa ujumla vyote vinalele watoto wasiopungua 40 kila kimoja. Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo bado wanamahitaji mengi japo kampuni ya simu za mkononi airtel imeweza kujitolea msaada huo wa vyerehani bado pia wanahitaji vifaa vya shule, vifaa vya kujifunzia, chakula pamoja na malazi ya kila siku.

 Airtel imekuwa mstari katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa   kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.bado Airtel inampango wa kutoa msaada wa cherehani pia katika mikoa ya mwezi huu kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa vituo vya wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.
Posted by MROKI On Thursday, August 04, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo