Meneja Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania TBL Fimbo Butallah akisalimiana na warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Ilala 2011 wakati wa uzinduzi wa kambi ya warembo hao leo
Warembo wafuatao kutoka katika katika vituo viwili vya Dar City Centre na Tabata wamefanikiwa kupitishwa na Kamati ya Miss Ilala kuingia kwenye kambi ya Miss Ilala inayo anza tarehe 4 Julai 2011. Warembo watakutana katika hotel ya Lamada Jumatatu saa nne kwa kwa ajili ya semina na kukamilisha taratibu zote za usaili ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba na Dar Metropolitan promotions.
Warembo hao ni:-
Jenifer Kakolaki, Alexia William,.Meryvine Kenzia,Patricia Kajubi,Salha Israel ,Lilian Paul, Diana John,Judith Mlingwa,Nasra Salim,Cresencia Haule,Godliver Mwashamba,Williet Wilson,Faizal Ally,Priscilla Mchemwa,Augostina Mshanga,Ritha Cuthbert,Lilian Bryceson,Maria John,Lilian William,Edna Mnada na Mariam Manyanya
Shindano la Redds Miss Ilala 2011 linategemewa kufanyika siku ya Vunja jungu katika ukumbi ulioko katikati ya jiji la Dar es salam.
Mpaka sasa hivi wadhamini waliojitokeza kudhamini Shindano hilo ni Redds Original inayozalishwa na kiwanda cha Tanzania Breweries Limited ambao ndio wadhamini wakuu, wengine ni Vodacom Tanzania, Tanzania Standard Newspapers, Fabak Fashion, TV Sibuka, Maisha Club, na 88.4 Clouds FM na Paris Pub ya Tabata.
Watakapokuwa kambini warembo watajifunza mambo mbali mbali yanayohusu mashindano ya urembo, mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kibiashara. Pia watajifunza namna ya kujitunza kama wasichana na kufanya shughuli za kijamii. Warembo pia wanategemewa kufanya michezo mbali mbali, kuonyesha vipaji na kufanya ziara ya kitalii.
0 comments:
Post a Comment