Nafasi Ya Matangazo

July 26, 2011

 Misa ya kumwombea Marehehemu Danny Mwakiteleko ilifanyika katika Kanisa hili la KKKT Usharika wa Ndala. Nabaade maziko kufanyika katika makaburi ya Masebe 1 kijijini Ndala, Kata ya Kandete, Tarafa ya Busokelo Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya. Danny alifariki Julai 23 na kuzikwa Julai 26, 2011.
 Baadhi ya wahariri waliohudhuria misa hiyo kanisani hapo...
 Wakazi wa Ndala, ndugu jamaa na marafiki waliohudhuria misa hiyo maalum.
 Meneja Mawasiliano wa Serengeti Breweries (SBL) Iman Lwinga (kushoto) na Mkurugenzi wa Habari wa Bunge, Jose Mwakasukwa nao walishiri.
 Mhariri Mtendaji wa New Habari, Deodatus Balile akisema machache juu ya Marehemu Danny...lakini alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi kanisani hapo.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda akitoa salamu za jukwaa hilo.
 Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya nao walisoma salamu zao.
 Bunge kupitia kwa Jose Mwakasukwa nao walitoa rambirambi zao.
 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jackson Msome  kwaniaba ya Serikali, alitoa rambi rambi zake.
 Zilifuata heshima kwa mwili wa marehemu Danny kutoka kwa familia yake, ndugu na marafiki.
 Mjane wa Bi. Winfrida akisaidiwa na rafiki zake baada ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu mkewe.
 Safari ya Makaburini ilifuata na Wahariri waliubeba mwili wa Mhariri mwenzao.
 Tayari mwili unashushwa kaburini...
Mkewe (juu) na Mama yake Mzazi Marehemu Danny wakiweka mashada ya maua kaburini. Hivi ndivyo ambavyo shughuli nzima ya mazishi ya Danny Mwakiteleko ilifanyika nyumbani kwako.
Posted by MROKI On Tuesday, July 26, 2011 1 comment

1 comment:

  1. Poleni wafiwa kwani yote ni kazi yake Mola. Apumzike kwa amani.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo