Nafasi Ya Matangazo

June 24, 2011

 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na watayaraishaji wa mitaandao ya mawasiliano ya Blogu, katika ukumbi wa sekretarieti, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam. Nape aliwaita na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya jamii na kufahamiana nao. Pamoja nae ni Katibu Mkuu Msaidizi Sixtus Mapunda.
 Baadhi ya wana Blogu ambao walihudhuria mkutano huo leo wakichukua dondoo.
 Nape akifafanua jambo katika mkutano huo hii leo. Akizungumzia zaidi kazi kubwa inayofanya na Blogaz katika ulimwengu wa sasa wa mabadiliko makubwa ya sekta ya habari.Kati ni Sixtus Mapunda na kulia ni Blogger, Mroki Mroki "Father Kidevu" ambaye ndie Director wa Blogu hii.
 Nape Nauye katika mazungumzo yake aliwashukuru sana Blogaz kwa kazi yao kubwa na ya ufanisi waliyoifanya katika kipindi cha Uchaguzio Mkuu wa 2010. Alisema Blogu zilikuwa zikitoa habari bila upendeleo wowote na zinaidadi kubwa ya wasomaji kuliko hata magazeti kwa sasa.
 Lakini Katibu huyu wa CCM aliwataka waandishi hawa wa Blogu wabaki na hali waliyonayo sasa ya aina ya uandishi ambayo anasema haipendelei wala kuonesha taarifa zao ni wazo la mtu fulani kama ilivyo kwa magazeti, na wasikubali kununuliwa wakawa na mrengo fulani wa uandishi.
 Pia aliwaomba sana Blogaz nchini kuwa mbali na kuangalia mapungufu yaliyopo katika utendaji wa serikali na Chama cha Mapinduzi nchini, amewaomba pia waangalie na yale mazuri yanayofanya na serikali hasa klatika kipindi hiki cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.
 Nape amesema, ni vyema Blogu zikaangalia enzi za mwalimu, wakati tunapigania Uhuru Tanganyika ilikuwa na nini katika sekta ya Elimu, Afya, Barabara, na mambo mengine kijamii na kulinganisha na sasa.
Mwisho alipata fursa ya kupiga picha na Blogaz hao.Ambao pia walimtaka awe anatoa ushirikiano wa karibu katika upatikanaji wa habari za chama, ili kuondoa taarifa zisizo na ukweli kutoka kwa vyanzo visivyo sahihi.
Posted by MROKI On Friday, June 24, 2011 1 comment

1 comment:

  1. AnonymousJune 24, 2011

    Una njaa kali mpaka unaudhi. Utabakia kutembea na malapa mpaka ukione cha moto

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo