UJUMBE wa wenyeviti na wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali za nchini Marekani umeanza kuwasili nchini ukiwa na lengo la kutengeneza diplomasia ya uchumi pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini.
Ujio huo ambao umeandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unafahamika kama V.I.P Safari ambapo kundi la kwanza la wakurugenzi hao limewasili jana majira ya saa 5:00 za usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)likitokea nchini Marekani.
Waliowasili jana ni pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE Electronic Corporation ,Bw J.Eric Pike na mkurugenzi wa kampuni ya CAMDEN Hospitality group inayojishughulisha na masuala ya Hotel ,Bw Munir Walji.
Ugeni mwingine ni Bw Ahmed Issa,rais wa kampuni ya Ahmed’s Moving Express,Inc ambayo pia ni wakala wa kampuni ya Wheaton World Wide Moving ikijishughulisha na masuala ya usafirishaji.
Ugeni huo utakuwa nchini kwa muda wa takribani siku 10 kuzungumza na viongozi mbalimbali akiwemo rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na rais wa Zanzibar ,Dk Ally Mohamed Shein.
Mbali na viongozi hao pia ujumbe huo unatazamiwa kula chakula cha pamoja na wafanyabiashara mbalimbali nchini kitakacho julikana kwa jina la Bussness Lunch itakayofanyika kesho mjini Arusha.
Mbali na hayo pia ugeni huo utakula chakula cha pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha na baadae utaendelea na safari ya kuelekea jijini Dar es salaam na kisha kuhitimisha safari hiyo kwa kutembelea Zanzibari.
Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw Suleiman akizungumza jambo na mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha umeme ya PIKE,Bw J,Eric Pike.

0 comments:
Post a Comment