Nafasi Ya Matangazo

May 27, 2011

Basi linaspringi za mbao zilizofungwa na mipira!
 Muda si mrefu imetokea ajali hii ya daladala T759AYE lilosajiliwa kufanya safari zake kati ya Mburahati na Kivukoni jijini Dar es Salaam lakini sasa linafanya safari zake kati ya Ukonga Mombasa na Moshibar/Kwamkolemba kupitia Mazizini,liliacha njia na kuingia mtaroni. Chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo kukata  "stelingi road" wakati likipandisha kilima cha Mazizini.
 Wakazi wa Mazizini Kata ya Ukonga na abiria walikuwamo katika gari hilo wakiangalia basi hilo katika eneo la tukio.
 Hii ndio Stelingi road iliyokatika na kusababisha gari hilo kuingia mtaroni.
 ..pia basi hili lilikata springi za mbele ambzo tayari zilikuwa chakavu na katika spring zilizotakiwa kuwepo ni moja tu ilikuwa inafanya kazi baad ya nyingine kuwa zilisha katika siku nyingi.
 Mbao zilizofungwa na mipira pia zilikuwa zikitumika katika basi hilo linalopakia abiria zaidi ya 30 huku wengine wakiwa wamesimama, jambo ambalo linawatia hofu watuamiaji wa vyombo vya usafiri kuwa je Askari wa Usalama barabarani wanayakagua magari haya au laa?
Hili ndo JACK LIVE likiwa limeacha njia, ajali hii haikusababisha majeruhi yeyote wala kugharimu maisha ya mtu zaidi ya chumka hiki chakavu kuzidi kuharibika.
Posted by MROKI On Friday, May 27, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo