Nafasi Ya Matangazo

May 10, 2011

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa, ulioanza jijini Istanbul Uturuki Mei 9, ukitarajiwa kumalizika mei 13 mwaka huu. Mkutano huo unahusu Maendeleo ya nchi masikini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo  na Balozi mdogo wa Tanzania  nchini Italia, Salvator  Mbilinyi, wakati wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Istanbul, Uturuki  walipo hudhuria katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi Maskini, ulioanza jana Mei 9, hadi Mei 13 mwaka huu.
Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiteta jambo na Balozi mdogo wa Tanzania  nchini Italia, Salvator  Mbilinyi, wakati wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Istanbul, Uturuki. Kulia ni Katibu  wa Makamu wa Rais , Zahor  Haji.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Msaidizi wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID), Donald K Steinberg (wapili kulia) na ujumbe wake wakati walipokutana kwa ajili ya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofsnyika jijini Istanbul Uturuki kuhusu maendeleo ya Nchi Maskini Duniani. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu.
Posted by MROKI On Tuesday, May 10, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo