Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2011

WAKAZI wa Kitongoji cha Kinyenze katika Kijiji cha Kipera Wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro huenda wakaingia katika mgogoro wa ardhi na mtu anaedaiwa kuwa ni mwekezaji anaetaka kuwekeza katika sekta ya kilimo cha ufugaji kuku Kitongojini hapo.

Mwekezaji huyo anaedaiwaa ni kaburu ambaye ni mmoja wa wazungu waliotimuliwa nchini Zimbabwe miaka michache iliyopita, anadaiwa kununua shamba lililokuwa likimilikiwa na Mtanzania Mwenye asili ya kiesia na mfanyabiashara wa mjini Morogoro, Badru D Walji.

Wakizungumza kwa njia ya simu kutoka kitongojini hapo baadhi ya wakazi hao wamesema Mzungu huyo amevamia mashamba ya kaya zaidi ya kumi na tano, kuingiaa katika maeneo ya nyumbaa za wananchi takribani kumi pamoja nae neo la makaburi.

“ Sisi tunashangaa kuona watu wanapita katika mashaamba yetu naa kuweka mawe ya mipaka na kudai kuwa eneo hilo ni mali ya Mzungu anakuja kuwekeza katika mradi waa ufugaji kuku,” alisema Mkazi mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa usalama wake.

Aidha mrokim.blog, ilimtafuta Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Enden Msangi na kutakaa kujua ukweli wa jambo hili alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo.

Aidha Msangi anasema kuwa wao kama Kitongoji na hata alipo wasiliana na uongozi wa kijiji cha Kipera kupata maelezo zaidi juu ya shamba hilo lenye ekari zaidi ya 250 kumilikiwa na Mzungu huyo ambae hata jina haalijafahamika waliambiwa Kijiji hakina taarifa zake.

Pia Msangi aliiambia mrokim.blog kuwaa tayari wameorodhesha majina ya wananchi wote waliokubwa na tatizo hilo na majina yamewasilisha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera kwa ufumbuzi zaidi japo bado kuna utata.

Hata hivyo baadhi ya wananchi hao wanamtaja Mwanakijiji Mwenzao David Guga kuwa ndie nyapara wa Mzungu huyo na ndie aliyepita kuonesha mipaka ya shamba hilo na kuingia katika mashamba mengine yasiyo husika.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho pia alisema mtu huyo tayari analalamikiwa na wanakijiji wengi kuwa amekuwa aakiwavuruga na hata alipoitwa katika vikao vya vijiji amekuwa akitoa vitisho hadi vya mauaji na hivi sasa anakesi Mahakama ya Mwazo Mikongeni ya kutishia kuua wanakijiji kadha akiwepo mwenyekiti huyo kwa mapanga.

Wananchi hao wameomba serikali kuingilia kati jambo hili mapema kabla halijaleta vurugu katika mashamba hayo ambayo pia inadaiwa Mwekezaji huyo anaweka uzio ambao utaziba njia za wakazi hao kwenda katika mashamba yao mengine na pia kufunga mawasiliano kati ya Kitongoji cha Kinyenze na Kile cha Mwanga kijijini hapo.

Mbali na kuiomba serikaali ya Wilaya na Mkoa kuingilia kati suala hilo wananchi hao wamesema watafanya maandamano hadi ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkoa kuwasilisha malalamiko yao hayo iwapo uongozi wa Kijiji hautalivalia njuga sakata hilo na wao kuachiwa mashamba yao.

“Miaka mingi tunajua mipaka ya shmaba hili la Muhindi, hata siku moja haijavuka barabara ndogo ya watembea kwa miguu iendayo Mwanga, sasa leo huyu Guga anamuonesha Mzungu kuwa mipaka inavuka mto ni ajabu,” alisema Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe

Taarifa zaidi zinadai kuwa mkazi ambaye alichuklua jukumu la kuonesha mipaka ya shamba hilo hadi kuvamia katika makazi yaw a tu, alifanya kukaribisha kijijini hapo miaka ya 90 na wala hajui mipaka halali ya shamba hilo ila kwa kuwa amezoea vurugu na ubabe wa jeshini alipofukuzwa ndo maana anafanya hivyo.

Blogu hii itaendelea zaidi kuwapasha yanayoendelea kujiri katika mgogoro huu na hatma ya mwekezaji huyo.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo