Mpoki akongozwa na Steven Kanumba mara baada ya kupokea tuzo yake ya wimbo bora wa asili katika wimbo wake wa Shangazi.
Mchezaji wa timu ya Simba Juma Kaseja na Taifa Stars (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Wimbo bora wa Taarab kiongozi wa bendi ya Jahazi Molden Taarab Mzee Yusuf, baada ya wimbo wa bendi hiyo kushinda katika tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award 2011, zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, kulia ni Mchezaji wa Yanga na timu ya Taifa Shadrack Nsajigwa.
Mtayarishaji wa muziki Man Water akipokea tuzo kwa niaba ya mwanamuziki 20% wakati wa utoaji wa tuzo hizo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mmoja wa maafisa wa Vodacom Foundation Mwavua Mlangwa akikabidhi tuzo kwa Popot mwakilishi wa mwanamuziki Lady Jay Dee ambaye hakuweza kufika katika utoaji wa tuzo hizo katikati ni Mkurugenzi wa Radio One Bw. Deo Rweyunga.
Tuzo hizo zimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi katikati akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa BASATA Gonche Materego kulia na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Angetile Osiah
Mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa Taarab nchini Bi. Kidude kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mwanamuziki Stara Thomas ambaye anaelekea katika muziki wa Gospel hivi sasa.
Mzee Yusuf wa pili kutoka (kulia)akifurahia pamoja na wanamuziki wa bendi ya Mapacha watatu mara baada ya wimbo wao wa Shida kushinda katika tuzo ya wimbo bora wa kiswahili. katika picha wengine kulia ni Josse Mara, kushoto ni Kalala Junior na wa pili kutoka kushoto ni Harid Chokoraa wote kutoka bendi ya mapacha watatu.
Waigizaji maarufu nchini Raymond Kigosi (kushoto)na Steven Kanumba nao ndani ya nyumba.
Mwigizaji Monalisa kulia akiwa akiwa pamoja na Consolata Miss Tabata 2010.
Mwana dada Lina kutoka kundi la THT akitumbuiza katika utoaji huo wa tuzo.
Mzee Mbagala nae hakubaki nyuma
Marlow nae aliwashika shati
Picha kwa hisani ya Full Shangwe
0 comments:
Post a Comment