Mtoto mlemavu Cornel Zagara akishirikia katika mbio za Vodacom 5KM Fun Run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanja.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr Noman Sigwa akimpatia zawadi Mtoto mlemavu Cornel Zagara aliyeshiriki mbio za Vodacom 5KM fun run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro,katikati Meneja Udhamini wa Vodacom Rukia Mtingwa.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr Noman sigwa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa Vodacom 5KM Fun Run Kalis Stiven kitita cha shilingi 100,000 mara baada ya kuibuka mshindi wa mbio hizo,kulia Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishangilia mara baada ya kumaliza mbio za Vodacom 5KM fun Run zilizofanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya washiriki wakitimua mbio za Vodacom 5KM Fun Run mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini Alhaj Musa Samizi kuanzisha mbio hizo.
ZAIDI washiriki 2000 wa rika mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wameshiriki katika mbio za Vodacom 5km fun run ambazo zimekuwa zikifana kila mwaka zikiwa ni sehemu za mbio za kimataifa za Kilimanjaro marathoni ambazo hufanyika kila mwaka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Katika mbio hizi za kujiburudisha ambazo zimekuwa zikipata washiriki wengi kila mwaka ,zimezidi kutia fora ambapo katika mbio hizo za jana alikuwepo mshiriki mdogo kuliko wote ambaye alikuwa kijana mwenye umri wa miaka mitatu wakati mkubwa kuliko wote alikuwa na umri wa miaka 70 ambao wote walipewa zawadi maalum na Vodacom.
Mgeni rasmi katika mbio hizo Mkuu wa wilaya ya Moshi Mjini Alhaji Mussa Samizi ambaye alizindua mbio hizo mapema jana asubuhi ameipongeza Vodacom Tanzania kwa kudhamini mbio hizo na kuiomba idhamini mbio za watu wenye ulemavu ambao zimesahaulika ambazo miaka miwili iliyopita zilikuwa sehemu ya mbio za Kilimanjaro lakini ziondolewa kwa kukosa mdhamini.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliitaka Vodacom kuzidi kuboresha mbio hizo ambazo zinapendwa na watu wengi wenye rika mbali hasa watalii ambao huja kushiriki mbio hizo na kufanya utalii pia jambo ambalo linaongeza pato la taifa na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando alitoa wito kwa Watanzania kushiriki kwa wingi katika mbio hizo badala ya kuacha mbio hizo kuwa na washiriki wengi zaidi wa nje kama ilivyozoeleka sasa kwani hivi riadhaa pamoja na kuwa mchezo pia ni ajira kwa upande mwingine.
Aidha Kamando alisema kuwa Vodacom imejipanga kuboresha zaidi mbio hizo za kilometa tano ingawa sio kwa kiwango kikubwa ili kutowavutia wakimbiaji wakubwa kuhamia kwenye mbio hizo kufuta zawadi endapo zitakuwa kubwa.
Washindi wa mbio hizo za Vodacom 5km walizawadiwa zawadi zifuatazo kwa wa wanaume na wanawake, mshindi wa kwanza akijinyakulia shilingi 100, 000,wapili shilingi 80,000,watatu shilingi 60,000,wanne shilingi 50,000,watano 40,000,na kuanzia mshindi wa tano mpaka wa tisa watapatiwa kifuta jasho cha shilingi 20,000 kila mmoja na kuwekewa muda wa maongezi kwenye simu zao wenye thamani ya shilingi 20,000.
“Pamoja na udhamini huu Vodacom inaamini kuwa itakuwa inaunga mkono juhudi za serikali za kunyanyua na kukuza vipaji vya wanamichezo hapa nchini ambao hapo baadaye wataweza kulitangaza Taifa letu katika nyanja za michezo za kimataifa.
Zaidi ya hayo tunashiriki mashindano haya ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali yetu za kukuza sekta ya utalii, hasa ukizingatia mashindano haya yanafanyika mkoani Kilimanjaro chini ya mojawapo ya vivutio vikuu vya utalii kama vile Mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimnjaro.
“Vodacom Tanzania itaendelea kudhamini michezo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza viwango vya michezo hapa nchini na hatimaye kuliletea taifa letu heshima katika mashindano ya kimataifa’.
Baadhi ya michezo inayodhaminiwa na na Vodacom ni pamoja na Mpira wa Miguu,Vodacom Miss Tanzania, mashindano ya kuogelea mbio za boti na mbuzi.
0 comments:
Post a Comment