Nafasi Ya Matangazo

January 15, 2011

 Makirikiri walipoanza show yao Usiku wa kuamkia Januari 15, 2010 katika kumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa Dar es Salaam.
 Staili hizi ziliwakosha sana wapenzi wa ngoma hizo za asili kutoka nchini Boswana.
 Wakazi wa Pugu Kajiungeni nao walikuja na kufurahia burudani hiyo ya aina yake kutoka katika kundi lililojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kutokanma na staili ya uchezaji wao na uimbaji.
 Hawa walijitokeza kucheza miondoko hiyo na mshindi alijinyakulia DVD na mshindi wa 2 alipata VCD huklu wa tatu akipata Maji ya Kunywa ya Kilimanjaro lita 1.5.
 Huyu alishika nafasi ya pili katika uchezaji....
 Huyu alishika nafasi ya tatu...
 Jamaa kati hapa ndio alikuwa mshindi wa show hiyo.
 Jamaa wakaendelea kuchochea mambo yao...
 Hapa ilikuwa kama wanataka kuendesha kibajaji ...
 Mambo yalinoga na hapa wakawa kama wanapanda pikipiki sasa...

 akina dada hawa nao walitia fora na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki..

 Makamnada wa FFU waliokojirani na ukumbi huo na hata wale wa JWTZ walioneshwa staili mpya ya kupiga kwata...
 Huyu alivutia sana kwa staili yake hasa ile ya kujibinya tumbo na kupandisha utumbo kifuani.
 Hapa ni mwendo wa kusakiziana...
 Mmoja mmoja alisonga mbele na kuonesha umahiri wake...
 Mashabiki walishindwa kukaa vitini na kuamua kunyanyuka...
Wachache walibahatika kupiga nao picha japo jamaa walikuwa hawataki kabisa jambo hilo lifanyike. Kundi hili ambalo lilikuwapo nchini kwa maonesho kadhaa tangu mwezi Decemba linataraji kuondoka nchini Januari 18 2011 kuelekea nyumbani kwao Boswana.
Posted by MROKI On Saturday, January 15, 2011 1 comment

1 comment:

  1. Ngoma za asili zina utamu wake. Hata kama sijasikia mapigo ya ngoma nk nimefurahi sana kuangalia hizi picha ahsante mzee kidevu!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo