Nafasi Ya Matangazo

January 24, 2011

 Ajali hii ya manzi kuangukia nyaya za umeme ilitokea Januari 23, 2011 huko Mji Mwema Kigamboni na kusababisha kukatika kwa umeme katika maeneo ya Kigamboni na Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mnazi huu uliopo kando kando ya barabara unaonekana kuwa umezeeka na kuliwa na wadudu jambo lililosababisha kuanguka kwake.
 Mafundi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco walifika katika eneo la tukio na kufanya jitihada za kuondoa mnazi huo.
 Iliwachukua saa kadhaa ili kufanikisha utatuzi wa tatizo hilo.
Vijana hawa wa Tanesco pia walishauri kufanyika kwa zoezi la kukata minazi yoye iliyo karibu na njia ya umeme ili kuepusha tatizo kama hilo kutokea tena kwani wanadai katika eneo hilo hii ni mara ya pili kunguka kwa mnazi.
Posted by MROKI On Monday, January 24, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo