Nafasi Ya Matangazo

July 07, 2026






Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na ugeni wake, wapo nchini Afrika Kusini, ikiwa ni ziara ya kikazi yenye lengo la kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha udhibiti wa upotevu wa maji ili kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Ziara hiyo iliyoanza Julai 6, 2026, imelenga kushiriki kikao kazi na wataalamu wa masuala ya teknolojia zenye uwezo wa kudhibiti upotevu wa maji, ili wananchi waweze kupata maji safi, salama na yenye kutosheleza kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Ikumbukwe kuwa, upotevu wa maji ni miongoni mwa changamoto inayoikabili Wizara ya Maji, ambayo imesababisha kupotea kwa maji mengi na kuzikosesha mapato mamlaka za maji katika wilaya mbalimbali nchini. 

Kimsingi, moja ya kipaumbele cha Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ni kupambana na upotevu wa maji. Hivyo ziara hiyo, ni mkakati wa kufanikisha kipaumbele hicho.

Katika ziara hiyo, Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Mwajuma Waziri, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana pamoja na wataalamu wengine wa wizara hiyo.

Pamoja na masuala ya maji, Julai 7, akiwa nchini humo, Aweso pamoja na ugeni wake wameshiriki kikamilifu hafla ya maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani. 

Katika hafla hiyo, amezindua Kituo cha Utamaduni wa Kiswahili Tanzania (Tanzania Kiswahili Cultural Center) ikiwa ni mkakati wa kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni ili kuendelea kukuza lugha hiyo na utamaduni wa Kitanzania ulimwenguni.
Posted by MROKI On Tuesday, July 07, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo