Nafasi Ya Matangazo

November 23, 2010

 Akina mama wakinadi bidhaa zao za kilimo kwa mteja aliye katika gari. 
 Licha ya ukame uliotawala katika maeneo mengi nchini lakini akina mama hawa wamefanikiwa kupata mazao haya na kuyauza kwa tabu kwa wasafiri ambao wakati mwingini hulazimika kuvamia magari yao pindi yasimamapo njia ya kuu ya Morogoro-Dodoma.
 Bidhaa kama hizi zingepatiwa soko la uhakika, wakulima wengi wangeondokana na umasikini uliopo na Kilimo ingekuwa ni eneo la ajira ambalo vijana wengi wangekimbilia tofauti na sasa.
Rais wakati analkihutubia Bunge mwaka 2010 katika Bunge la kumi, katika moja ya vipaumbele vyake 13 ni masoko ya uhakika ya mazao ya kilimo na kuwainua wakulima na jembe la mkono. Likitimia hilo hakika tanzania itakuwa ni mahala pazuri sana kuishi na Kilimo ndio itakuwa ajira pekeee ya uhakika nchi hii. 
Posted by MROKI On Tuesday, November 23, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo