Wananchi wa Kijiji cha Kijungu Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara, wakimsikiliza mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimpongeza mkewe Bi Asha Bilal, baada ya kutunukiwa na muvishwa vazi la asili la kabila la Kimasai, wakati walipofika kwenye Uwanja wa Kijiji cha Kijungu Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara kufanya mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kijungu Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo
Wananchi wa Kijiji cha Kijungu (Wamasai) wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana Okt 7, Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kiteto, Benedict ole Nangolo, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara
Mgombea Mwenza wa Uris wa CCM, DK. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia alikuwa ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Kiteto na ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wa Dk. Bilal Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Fatma Mrisho, baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kijungu Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.
Dk Bilali na mkewe Bi Asha Bilal, wakitoka kwenye Uwankja wa mkutano baada ya kumaliza mkutano wa kampeni Kiteti.













0 comments:
Post a Comment