Watembea kwa miguu wamekuwa wakiathirika sana na wanahitaji msaada wa Trafiki hasa pale ambapo wanaona usalama wao kutoka kwa madereva wazembe ni wamashaka. Pichani ni Askari wa Usalama barabarani Unguja kisiwani Zanzibar akimvusha Mzee mkazi wa mji huo barabara ili asije kugongwa na magari au watumiaji wengine wa barabara hiyo karibu na kituo cha daladala darajani.
Trafiki wanapaswa kusimama sehemu za vivuko vya watembea kwa miguu na kuwasaidia watu wa rika mbalimbali kuvuka hasa watoto na wazee kama hawa ili kuepusha ajali zisizo za msingi tofauti na askari wengi kukalia kukamata madereva tu na kuwatoa kitu kidogo jambo ambalo linawachafua askari hao wenye dhamana ya usalama barabarani.






0 comments:
Post a Comment