Nafasi Ya Matangazo

August 05, 2010

Uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge nchini Tanzania umekaribia kabisa na tayari kila chama cha siasa kimesha teua wagombea wake na wengine kuanza kampeni za hapa na pale katika kuhamasisha wanachama wao kujitokeza kupiga kura na pia kuhamasisha wasio wanachama kujiunga na chama chao.
Pichani ni moja ya tangazo la kijiweni huko Kigoma mwisho wa reli ambalo limeanza na kichwa "THE VOICE OF PEOPLE IS THE VOICE OF GOD" yaani SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU.
Kisha ujumbe huo hapo chini:-TANGAZO TUNAPENDA KUWATANGAZIA WANAKIJIJI WA KIGOMA UKIWA NA KADI YA CCM UKIENDANAYO SOKONI KILA BIDHAA UTAPUNGUZIWA BEI, KAMA UNGA-SUKARI, MCHELE-MAHARAGE-MKAA MRADI UONESHE KADI YA CCM NA UMEME UTAWAKA KWAKO. HIYO NI KWA WANA CCM TU WENYE KADI HAI. CCM OYEEEE!!!
Posted by MROKI On Thursday, August 05, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Hilo tangazo ni la udhalilishaji! je baada ya hiyo hongo ya kura, umasikini si ni kama kawa! watanzani tusiuze uzalendo kwa bei poa hivyo.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo