Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2010

Klabu kongwe ya makapera wa Kampuni ya Cargo Stars imepata pigo baada ya mwanachama wake chipukizi na machachari Ramadhani Hussein kuamua kuihama klabu hiyo na kuingia klabu ya wanadoa kwa kufunga ndoa na Bi Joha Salum.
Pichani ni Maharusi hao Ramadhani na Joha wakiwa na nyuso za furaha wakati wa tafrija yao ya ndoa iliyofanyika Dar es Salaam Agosti 6 2010 katika Ukumbio wa Makete. Bwana harusi ni mfanyakazi wa Kampuni ya Cargo Clearence ya Dar es Salaam.
Baadhi yawafanyakazi wa Cargo wakiserebuka na Bwana harusi.
Ramadhani akiwa katika misosi na mkewe Bi Joha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Cargo wakiwa katika picha ya pamoja na Maharusi na wapambe wao.
Hawa ni wadau wa Oysrebay Alliance ambao walipiga kitabu pamoja na Bwana harusi mwaka 1992-1998 pale Obay Primary.

Posted by MROKI On Saturday, August 07, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo