Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2010

Mwanachama wa CCM wilayani Maswa na mgombea Ubunge wa jimbo la Maswa Magharibi, Jidula Mabambasi amedaiwakufariki dunia Agosti 2 2010 asubuhi wakati akisafirisha kuwahisha Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu.
Mabambasi atakumbukwa katika medani za siasa kwani ndiye aliyewahi kumng'oa uenyekiti wa UDP John Momose Cheyo baada ya kufanya mapinduzi Baridi.
Mabambasi alizidiwa Jumamosi siku ya mwisho katika kampeni na kukimbizwa Hospitali ya wilaya ya Maswa ambako alilazwa hadi Jumatatu kwa matibabu lakini hali yake ilivyozidi kuwa mbaya alikimbizwa Hospitali ya rufaa lakini bahati mbaya alifariki dunia kiwa njiani.
Chanzo Wanabidii.net
Posted by MROKI On Tuesday, August 03, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo