Mustafa Hassanali pamoja na Msaidizi wake Hamiss (kulia) wakiangalia picha zilizochorwa na Wagonjwa wa Akili katika Hospitali ya wagonjwa hao Visiwani Zanzibar.
Mbunifu wa Mitindo maarufu nchini Tanzania na dunia, Mustafa Hassanali akiangalia moja ya magodoro yaliyopo katika Wodi ya wagonjwa wa akili ya Zanzibar hivi karibuni wakati alipotembelea Hospitali hiyo muda mfupi kabla ya kuendesha Onesho la Mavazi la kuchangia Fedha Hospitali hiyo ambayo inakabiliwa na uhaba na mahitaji ya vitu vingi.
Hassanali alisikitishwa na hali iliyopo katika sehemu hizo za kulala wagonjwa hao na kuahidi kuwasiliana na marafiki zake mbalimbali ili kuona vile watakavyoweza kusaidia ikiwa ni pamoja na kupiga rangi kuta na kununua magodoro mapya.
Mroki eeh!
ReplyDeleteHivi huyo Mustafa Hasanali amekula dawa ya Dokta Ndodi gani mpaka ametrim mno sana kiasi hicho?
Tunaomba sana umuombe asiwe Mchoyo atufahamishe na sie kwani tuko wengi ambao tuna hayo maunene na hatuyapendi na tungependa kupyapunguza.
Asiwe mnyimi wa Elimu. Atugawie na sie hiyo elimu tafadhali