Nafasi Ya Matangazo

July 14, 2010

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Cleopa David Msuya akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa Dar es Salaam leo.
Mmoja wa wanahisa akiuliza swahi na kutaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa kampuni hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Cleopa David Msuya (kushoto) akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wanahisa Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goet szche na kushoto ni Mwanasheria wa TBL Huruma Ntalena.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goet szche akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wanahisa wa Kampuni ya Bia TBL Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya TBL Cleopa David Msuya na Kulia ni Mzee Anorld Kilewo.
Baadhi ya wanahisa wakipata chai baada ya mkutano huo leo.


Baadhi ya wadau wa TBL wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Wanahisa Dar es Salaam leo.
Mkuu Mpya wa Kitengo cha PR na Communication wa TBL, Bi Editha Mushi alipotambulishwa rasmi kwa waanahabari leo. Editha amechukua nafasi ya Maneno Mbegu ambaye amejiuzulu kwa mujibu wa sheria baadaya kutangaza nia ya kuwania Ubunge jikbo la Kisarawe.
*******
KAMPUNI YA BIA TANZANIA-TBL YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA NA WANAHISA JIJINI DAR ES SALAAM.

Dar es Salaam, Julai 14, 2010: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka na wanahisa wake ili kujadili maazimio mbalimbali ya juu ya uendeshwaji wa kampuni.
Akiongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Kempinski jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Mawasiliano wa TBL, Bw. Steve Kilindo alisema, “Huu ni mkutano mkuu muhimu sana kwa kampuni yetu; wahahisa wa TBL wamekusanyika hapa leo kujadili maswala ya msingi yahusuyo biashara ya kampuni.
Pamoja na mambo mengine, wanahisa wataombwa kupitisha kumbukumbu za Mkutano Mkuu uliopita wa kampuni wa tarehe 15 Julai 2009, na pia kuidhinisha Ripoti ya Fedha na ya Wakurugenzi”

Aliendelea kwa kusema kuwa “mkutano huu pia utatoa ruhusa ya kulipwa gawio la Tsh 150 kwa hisa za kila mwahahisa kwa mwaka wa mahesabu ulioishia tarehe 31 Machi 2010, pamoja na kuteuliwa kwa kampuni ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Ms PriceWaterHouseCoopers, kama wakaguzi kisheria wa mahesabu ya kampuni yetu kwa mwaka utakaoshia tarehe 31 Machi 2011”.

Rekodi nzuri ya utendaji kifedha ya Kampuni ya Bia Tanzania-TBL imeendelea kukua kwa mara nyingine tena katika miezi 12 iliyopita iliyoishia tarehe 31 Machi 2010, pamoja na kwamba kulikuwa na ongezeko la gharama za uzalishaji, ushindani na pia mazingira ya hali ya uchumi.
Mapato kutokana na mauzo yaliongezeka kwa asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka uliopita, kutokana na kufanya vizuri katika soko pamoja na kuimarika kwa kiwanda kuwa na bidhaa nyingine za viwango vya juu katika soko.

Fedha iliyopatikana kutokana na shughuli za uendeshaji ya kiasi cha Tsh 165 bilioni kina akisi ongezeko la 45% zaidi ya mwaka uliotangulia. Fedha zilizotumika kulipia kodi ya shirika na faida ilifikia kiasi cha Tsh. 45 bilioni na Tsh 113 bilioni zilitumika kulipia matumizi ya mtaji, ambapo bilioni 47 zilizobaki zilitumiwa kulipia gawiwo kwa wana hisa.

Kampuni iliendelea kujikita katika kujipanua na program mahsusi ya kustawisha majengo ya viwanda. Katika mwaka, kiasi cha Tsh. bilioni 113 ziliwekezwa katika program hii ambayo ilihusisha ujenzi na ufunguzi wa kiwanda kipya cha bia cha Mbeya pamoja na mitambo mipya ya kujazia bia jijini Dar es Salaam.

Pamoja na fedha zilizohitajika kulipia gharama za program ya upanuzi wa kiwanda, Bodi iliidhinisha pato la gawio kwa wanahisa la jumla kwa mwaka liwe Tsh 150 kwa hisa. Gawio kwa wanahisa limekuwa likilipwa kwa awamu ya kwanza na pili kwa Tsh 60 na Tsh 90 kwa kila hisa. Gawio la pili lililipwa kwa jumla badala ya gawio la mwisho na Bodi ilipendekeza hakuna gawio jingine kwa mwaka huu wa fedha.

Posted by MROKI On Wednesday, July 14, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo