Nafasi Ya Matangazo

July 06, 2010

Baadhi ya wasanii chipukizi walioweza kujizolea majina ambao watashiriki Tamasha kubwa la Burudani Mwaka huu la FIESTA JIPANGUSE litakalo anza Julai 7 mjini Morogoro. wadao kutoka Clouds FM na Clouds TV wakilamba snap wakati wa kutambulisha wasanii hao Dar es Salaam jana.
Rasta Mnene Tanzania ambaye sasa yupo ndani ya familia ya Clouds TV akibadilishana mawazo na mwenzake.

Tamasha la FIESTA JIPANGUSE 2010 litaanza mjini Morogoro na baade kwenda Mkoani Arusha Julai 9 katika Ukumbi wa Matongee Club na baade Mkoani Kilimanjaro katika ukumbi wa Laliga Club Julai 10.

Julai 16 Fiesta Jipanguse itawatoa vumbi wakazi wa Mji wa Dodoma katika ukumbi wa Royal Vilage usiku na kisha Julai 17 katika uwanja wa Jamhuri mchana kutakuwa na show kabambe ya kuwapangusa vumbi wanafamilia.


Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwawani wagosi wakae tayari kwani Julai 24 wao watajipangusa na Fiesta kabla ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake kupata wasaa wa kujipangusa mwiosho wa mwezi Julai.

Safari ya Fiesta itaelekelea Zanzibar na Musoma Agosti 6 katika ukumbi wa Musoma Hotel kabla ya kufungwa Agosti 8 katika jiji la Kandoro Mkoani Mwanza.

Wasanii 30 watashiriki tamasha la mwaka huu ni wakiwamo Diamond, Belle 9, Hussein Machozi, Baby J, Offiside Trick, Chege & Temba, Shaa, Juma Nature, Dully Sykes, Barnaba, Amini, Linah, Godzilla,Joh Makini, Roma, Kiki wa Pili, Young Dee, Fid Q, Mwana FA, Mataaluma, JCB, Tip Top, Mwasiti, Pina na Beatrice.
Posted by MROKI On Tuesday, July 06, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo