Nafasi Ya Matangazo

July 19, 2010

Lori la mizigo Semi Trela T867AEJ na tela lake T921AAM lililopata ajali jana mchana eneo la katikati ya Kabuku na Segera barabara kuu ya Chalinze-Segera baada ya kugongana na Land Cruser T196ANQ yote yakitokea Chalinze kuelekea Segera.
Land Cruser T196ANQ ambalo kwa mujibu wa dereva wa derev wa lori ni kuwa baada ya kuwapita likasimama ghafla mbele yako katika mlima na gungongwa kwa nyuma na yote mawili kupinduka bondoni.
Mtu anae daiwa kuwa ni dereva wa Land Cruser T196ANQ akijaribu kuinuka bila mafanikio na kulalamika maumivu makali sehemu ya shingo na mgongo.
Mzungu aliyekuwa katika Land Cruser T196ANQ akiwa taabani baada ya kuumia vibaya sehemu ya kichwani.
Mmoja wa watoto wa dereva wa lori akiwa katika gari kupelekwa Hospitali baada kuvunjika mkono.
Dereva wa Lori akiwasiliana na tajiri yake ili kutuma gari lingine kuhamisha mzigo waliokuwa wakisafirisha. Dereva wa Lori akiwa amejeruhiwa vipaja katika mgongo wake na kulalamika maumivu makali sehemu ya kifua.
Tandiboi wa Lori la Mizigo akiwa amepata majeraha kichwani na mkononi.
Mke wa Dereva wa Lori akiwa amekumbatia watoto wake wakipelekwa Hospitali.
Majeruhi wakiwa katika gari kupelekwa Hospitali.
Mmoja wa Askari wa JWTZ waliokuwa wakipita eneo la ajali na kutoa msaada kwa majeruhi na kulinda malizao ambazo wananchi walitaka kuwavamia na kuwaibia hadi Polisi walipofika.Gari walilokuwa wakisafiria Wanajeshi wa JWTZ waliotoa msaada wa kuwanasua majeruhi katika magari na kulinda mali zao. Wanajeshi hawa wanastahili pongezi kwani wanadai walipambana na wananchi waliokuwa wakitaka kuiba.

Posted by MROKI On Monday, July 19, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo