Mfanyabiashara ndogo ndogo wa Mwanza, Bwana Jumanne Seke akichangia kampeni maalum ya ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia wanafunzi wenye ulemavu inayoendeshwa na TEA pembeni ni Afisa Uhamasishaji na Ukuzaji Rasilimali Bwana Godfrey Massawe.
Wananchi wenye kiu ya taarifa za elimu kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wakiwa wamefurika kwenye banda wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari Elimu na Mawasiliano wa TEA Bi Caroline Manoni katika maonyesho ya Utumishi wa umma yanaondelea katika viwanja vya Kirumba Mwanza.
Mtoto Joseph Kulwa akiwa pamoja na Meneja Habari Elimu na Mawasiliano wa TEA Bibi Sylvia Lupembe Gunze ndani ya banda la TEA katika maonesho ya wiki ya utumishi yanaoendelea katika viwanja vya Kirumba Mwanza.
Bi Sofia Zakaria na nduguze, Siwema Zakaria na Kashidye Zakaria wakisililiza maelezp juu ya kazi na majukumu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania kutoka kwa Afisa Uhamasishaji na ukuzaji Rasilimali wa TEA Bwana Godfrey Massawe.
Wanafunzi kutoka shule ya Msingi Nyamanoro wakisoma jarida la TEA walipotembelea banda la TEA katika maonesho ya wiki ya utumishi viwanja nya Kirumba Mwanza, Mkaguzi Mkuu wa ndani wa TEA Bi Fatuma Chillo nyuma yao akiwaongoza.
0 comments:
Post a Comment