Nafasi Ya Matangazo

June 09, 2010

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu anayeshughulikia Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame akitoa muhtasari wa mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Zanzibar.
WANANCHI wakiwa wanaangalia ajali iliotokea katika barabara ya Michezani, mpanda baskeli aliigonga daladala kwa nyuma baada ya kusimama kwa hafla mbele yake, mpanda maskeli huyu ameumia na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
ASKARI wa Usalama barabarani akiwa na Pikipiki ambayo ameikamata kwa makosa ya barabara akiikokota kuipeleka Kituo cha Polisi Malindi, kama alivyokutwa na mpiga akikatisha mitaa ya Darajani.
WACHUKUZI wa mizigo wakiwa na rumbesa ya mzigo wakikatisha katika mitaa ya Darajani Unguja, uchukuzi wa namna hii unaweza kuleta madhara kwao kutokana na kutoona kinachotokea nyuma yao.
WAKAZI wa mji wa Unguja wakijipatia mahitaji ya vitu vya nyumbani katika mnada wa marikiti darajani, tafauti na zamani katika mnadfa huu vilikuwa vikuuzwa vitu vikongwe.

Posted by MROKI On Wednesday, June 09, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo