Nafasi Ya Matangazo

May 06, 2010

Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuwa mgeni rasmi Miss Arusha City Center
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Eng. Raymond Mushi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro cha Vodacom Miss Arusha City Center inayofanyika kesho katika ukumbi wa hoteli ya Naura Springs.

Akifafanua katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi huo, Mkurugenzi wa Sophy Entertainment, Sophia Urio ambao ni waandaaji wa kinyang’anyiro hicho alisema kuwa kwa sasa wamejipanga vyema.


“Tunashukuru sana waandishi wa habari ambao wamekuwa bega kwa bega na sisi katika kufanikisha hilo ambalo linatarajiwa kuanza kesho saa 1 usiku na kumalizika saa 6 usiku.Kampuni yetu ndiyo ya kwanza kwa mkoa wa Arusha kufungua mashindano ya Vocodacom Miss Arusha City Center na kufuatiwa na vitongoji vingine.


“Tunamshukuru Mungu tumepata washiriki wenye mvuto mbele ya jamii na tunaamini shindano letu litakuwa na ushindani na msisimo”. Alisema Sophia”.Kwa sasa tunao warembo 11 hao wapo kambini wakijinoa tayari kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.


Mataji yatakavyoshindaniwa ni Vodacom Miss Arusha City Center na Balozi wa Naura Springs Hotel.Wasanii watakaotumbuiza katika onyesho hilo ni Kikundi cha ngoma za asili kiitwacho Perfect Youth Group, Bendi iitwayo Aqua Sound na wasanii wengine ni Hussein Machozi huyu ni msanii wa hapa Tanzania.


Tunawashukuru sana wadhamini wetu ambao ni Vodacom, Naura Spring Hotel, Little Roses, Aqua Sound, Shuphaa Quality Boutique, Janneth Beauty Parlour. Warembo wakijifua tayari kwa shindano hilo.
Posted by MROKI On Thursday, May 06, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo