Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza rais Jakaya Kikwete leo alipozungumza nao na kulihutubia taifa.
Rais Kikwete katika mazungumzo yake hii leo alizungumzia mambo makuu mawili. Awali alizungumzia kufanyika kwa Mkutano Mkubwa wa Kujadili Uchumi Duniani kwa Bara la Afrika (World Economic Forum for Africa) unataraji kuwanyika Dar es Salaam kwa siku tatu Mei 5-7 2010 na viongozi wa nchi 11 wataanza kuwasili nchini kuanzia kesho.
Kufuatia mkutano huo Rais amewaomba watanzania hasa wakazi wa Dar es Salaam kwa usumbufu utakao jitokeza kwa njia kadhaa kutumika zaidi na wageni wa mkutano huo.
PILI: Rais Kikwete alizungunmzia vuguvugu la kmgomo wa wafanyakazi nzima ambao unashinikizwa kuwapo na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA na kusema mfanyakazi wa serikali atake goma atakuwa amepoteza haki zake zote.
Amewasihi wafanyakazi kutoshiriki katika mgomo huo kwani viongozi wa TUCTA wameafikiana mambo kadhaa wa kadha katika vikao lakini wakitoka wanapotosha licha ya kusaini makubaliano hayo.
Kifupi amesema serikali haiwezi kubaliana na madai ya TUCTA kuwa wafanyakazi wa aina zote mshahara uwe 315,000 kwa kima cha chini.
Na wale wanasema kuwa hawataichagua CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa serikali yake haijali wafanyakazi amsema waache wasichague maana serikali haiwezi neemesha wachache na watanzania wengine kuteseka hasa walio vijijini.
Sio kweli kuwa serikali haina pesa za kuwalipa wafanyakazi..wao(walio madarakani)wanalipana mamilioni ya shillingi kwa kazi wasizofanya..halafu wanakuja hapa ktk magari ya serikali kuleta dharau na kiburi kwa watu waliowapa ulaji(waliowachagua).Hotuba ya raisi imejaa vitisho,dharau na jeuri ya hali ya juu.mi nafikiri ni wakati umefika kwa hawa watu wa ccm kupata reality check;vote them out!
ReplyDelete