Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2010

Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania ( TUCTA), Omari Juma (kushoto) akiweka vizuri tamko alilolisaini la ufafanuzi wa notisi ya mgomo wa wafanyakazi wote iliyotolewa na Shirikisho hilo mara baada ya kikao cha dharura cha Kamati kuu ya utendaji wa TUCTA kilichokutana jana mjini hapa , Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA , Nicholaus Mgaya.

SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema mgomo upo pale pale pamoja na vitisho vilivyotolewa na Chama cha Wajiri Tanzania (ATE) na wale wote wanaopinga mgomo huo kwani ni halali kwa mujibu wa sheria na mahusiano kazini.

Pia TUCTA imesema kuwa ipo tayari kuingia katika meza ya majadiliano na Serikali lakini imeitaka kutambua majadiliano hayo hayataingiliani na mipango na mikakati inayoendelea ya kutekeleza azma ya kugoma na kwamba mgomo huo utasitishwa iwapo meza ya majadiliano itatoa makubaliano ya utekezaji wa madai ya wafanyakazi.

Tamko hilo limetoloewa jana mkoani hapa na Rais wa TUCTA Omari Juma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati kuu ya utendaji ambapo aliwataka wafanyakazi kutotishika na vitisho vyovyote na chama cha wajili nchi kwa kuwa hadi sasa haijapokea taarifa ya maandishi kutoka mamlaka halali iliyowekwa kisheria kubatirisha notisi ya mgomo.

Alisema pamoja na hotuba ya rais kugusia mishahara tu na kuacha madai ya wafanyakazi juu ya upunguzwaji wa kodi ya mapato (PAYE) na kutotaja mahitaji ya wafanyakazi juu ya mafao bora yanayotakiwa kutolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii wameamua kuingia katika majadiliano kutokana na rai iliyotolewa na rais kuonyesha kutatua madai yao ya muda mrefu.

Rais huyo wa TUCTA alisema kuwa mgomo huo uliotishwa hauna uhusiano wowote wala ushawishi wa chama chochote cha kisiasa kama inavyodhaniwa na kutangazwa na baadhi ya wanasiasa.

Aidha alisema kuwa tamko hilo la mgomo bado ni halali kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 85 (6) ambapo kinawapa mamlaka vyama vya wafanyakazi kuitisha mgomo .

Akizungumzia ATE ,rais huyo wa TUCTA alilaani tamko la chama hicho na kauli zake za vitisho kwa wafanyakazi wanyakazi wanyonge wanaotumia haki yao ya kugoma kupigania haki zao za msingi zinazonyonywa na waajili.

Alisema kuwa TUCTA inahamini sababu saba za tamko la mgomo zilizowasilishwa kwenye baraza la kazi uchumi na jamii (LESCO) zinalenga kueleza madai matatu ya msingi ya wafanyakazi ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakiwasilishwa Serikalini.

Ameyataja madai hayo kuwa ni ongezeko la kima cha chini cha mshahara kufikia 315,000 ,kupunguziwa kodi ya mapato inayokatwa katika mishahara ya wafanyakazi pamoja na kudai mafao bora ya uzeeni kutoka katika mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo nchini.

Kuhusu wito wa rais ,TUCTA imesema hawanabudi kumkubusha kuwa wafanyakazi wamekuwa wasikivu na wavumilivu huku wakitambua kuwa amani na utulivu sehemu za kazi ndio nguzo muhimu za kuongeza tija na kukuza uchumi wa nchi na kwamba madai yaliyowasilishwa katika notisi hiyo ya mgomo sio mapya na kwamba hayajapatiwa ufumbuzi unaokusudiwa na wafanyakazi.

Rais huyo wa TUCTA aliendelea kusema kuwa madai yamekuwa yakiwasilishwa kila mwaka katika hotuba za maadhimisho ya sherehe za mei mosi kwa Rais na daima yamekuwa ya ahadi za ushughulikiaji .
Posted by MROKI On Sunday, April 11, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo