Ukuta uliotobolewa
Watu wasio julikana wamevamia Nyumba Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk Ramadhani Dau iliyopo Kinondoni Dar es Salaam na kutoboa ukuta na kuiba.
Watu hao kabla ya kutimiza adhma yao hiyo waliwafunga kamba walinzi wawili wa nyumba hiyo, Deus Mtatilo (52) na Yusuf Bakari (56) kisha kuiba Kasha la kuhifadhia fedha na nyaraka nyingine mali ya Dau.
Taarifa za Kipolisi kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, zilizotolewa na Kamanda Elias Kalinga zinasema tukio hilo lilitokea saa tisa usiku huku Dau na familia yake wakiwa nje ya nyumba hiyo kwa mtoko wa kawaida.
Tundu ndo hili
“ Kwa mujibu wa maelezo ya walinzi ambao walikuwa na jukumu la kulinda nyumba hiyo ni kuwa watu wasiojulikana walitoboa na kwenda kuwafunga kabla ya kuvunja nyumba na kufanya huarifu" alinukuliwa Kalinga.
Aidha Polisi wanasema kilichoibiwa ni nyumbani hapo ni sefu ambayo ilikuwa na fedha, ingawa amesema kuwa mwenyemali (Dau) hakumbuki kulikuwa na kiasi gani cha fedha kilikuwemo katika sefu hiyo.
Polisi inawashikilia walinzi hao hasa kutokana na mashaka Jeshi hilo iliyonayo kutokana na jinsi tukio lilivyotokea..., "haiwezekani walinzi wenye bunduki zenye risasi kadhaa waache watu watoboe ukuta na kwenda kuwafunga kamba bila hata kuwarushia risasi na ndio maana tunawaona kuwa ni washukiwa wa kwanza kuwa wanawezekana kuwa wamekula njama watu wengine.
Ukuta huu una nyaya za umeme juu.
KWA MSHAHARA GANI HALALI WA KUJENGA NGOME KAMA HIYO.
ReplyDeleteWACHA WAIBIWE NA WATAIBIWA SANA KADRI MWANYA WA MASIKINI NA WALIONACHO UNAVYOZIDI KUKUWA.
NDO MAANA UJAMBAZI UTAZIDI.
UMASIKINI NDO CHANZO CHA WIZI NA UJAMBAZI.
KAMA SERIKALI HAITASAIDIWA WATU KUONDOKANA NA UMASIKINI BASI WATAIBIWA SANA TU.