Habari zilizoifikia Blogu ya Watu hivi Punde zinasema kuwa MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Aloyce Kimaro ameugua gjhafla akiwa mjini Dodoma anakohudhuria kikao cha Bunge jana jioni na amesafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhumbili kwa Matibabu zaidi hii leo.
Akizungumza na Wandishi wa habari leo, Kaimu Mganga Mkuu, Dk. Philemon Saigod wa Hospitali ya Mkoa Dodoma amesema Kimaro anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi.
Aidha habari kutoka Dodoma pia zinasema Kimaro alidondoka akiwa Viwanja vya Bunge na kukimbizwa Hopitali ya Mkoa Dodoma kwa matibabu jana.
Spika wa Bunge Samuel Sitta amewatangazia Wabunge juu ya Hali ya Mbunge Mwenzao kuwa, Kimaro alikimbizwa Hospitali jana na kugundulika kuwa anakiharusi kidogo na anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.
Blogu hii iataendelea kuwapa taarifa zaidi juu ya tukio hili.
Mbunge Kimaro ni miongoni mwa wabunge waliopo mstari wa mbele katika kupigavita ufisadi.
0 comments:
Post a Comment