Nafasi Ya Matangazo

April 28, 2010

Lori aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 757 BGV, limepinduka na kusababisha vifo vya wanachuo 16 papo hapo kwenye mzunguko wa barabarani.

Katika ajali hiyo, wanachuo wengine 125 wa Chuo cha Kiislamu cha Sghanmsi Maarifa jijini hapa walijeruhiwa.

Lori hilo lilidaiwa kubeba zaidi ya wanachuo 140 kilichoko mtaa wa Majengo jijini hapa, wakati wakirudi
mjini kutoka kijiji cha Kibafuta, kuhudhuria Maulid.

Ajali hiyo ilitokea juzi saa 5.30 usiku katika eneo la mzunguko wa Mabanda ya Papa katika barabara ya 21 mjini hapa ambapo lori aina ya Mitsubishi Fuso namba T 757 BGV lilipinduka.

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Bombo, Dk. Fred Mtatifikolo, muda mchache baada ya ajali hiyo, walipokea maiti 14 na majeruhi 125 na kati yao majeruhi wengine wawili walikufa wakihudumiwa hospitalini hapo.
Alisema hadi jana mchana, maiti wote walitambuliwa na ndugu zao, huku majeruhi 70 kati ya 125 waliruhusiwa kurudi nyumbani kutokana
na afya zao kuendelea vizuri.
Posted by MROKI On Wednesday, April 28, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo