Nafasi Ya Matangazo

April 19, 2010

Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali leo ameenguliwa rasmi katika orodha ya wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ya Simba katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika baade mwezi ujao.
Dadali alienguliwa leo wakati Kamati ya Uchaguzi ya Simba kuketi leo katika ofisi za TFF Ilala Dar es Salaam na kupitia na kuwahoji wagombea mmoja baada ya mwingine.
Kwamujibu wa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Damas Ndumbaro amesema Dalalai hakutimiza vigezo vya kugombea uongozi Simba ambapo Mgombea anatakiwa walau awe na elimu ya Kidato cha nne.
Pamoja na Dalali Mwingine aliyekubwa na tatizo hilo ni na kuenguliwa ni Mohamed Nyalali.
Hivyo sasa nafasi ya Uenyekiti wa Simba Ismail Rage, Hanspope Zacharia, Michael Wambura, Hassan Hassano na Andrew Pupa.
Posted by MROKI On Monday, April 19, 2010 3 comments

3 comments:

  1. ...Je kigezo cha elimu kipo kwenye katiba ya Simba? Kama kipo ilikuwepo Bw. Dalali akapewa fomu?
    Migogoro mingine kwenye klabu tunaitafuta wenyewe kwa kutozingatia katiba na kanuni zinazoendesha klabu hizi...

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu wala hawa jamaa wa Simba hawajakosea Kigezo cha elimu kipo katika Katiba Mpya ya Simba na Dalali mwenyewe alipitisha hilo kuwa walau Kiongozi wa simba awe na Elimu isiyopungua kidato cha Nne.

    Hivyo imeanza kula kwake.

    ReplyDelete
  3. simba walimchagua vipi dalali huko nyuma.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo