Magari yaliyogonganaWakazi wa Mwanga wakishuhudia uokoaji
Basi lilolohusika katika ajali.
Basi lilolohusika katika ajali.
Magari yalikwama kwa muda
Ajali
MTU mmoja amefariki dunia papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la daraja la mto kifaru wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mawenzi na KCMC na kwamba aliyefariki ni fundi mitambo wa lori ambapo jina lake bado halijafahamika.

Ajali hiyo iliyolihusisha gari la Rombo Express lenye namba za usajili T255 AHV lililokuwa likitokea Rombo kwenda jijini Dar es salaam na Lori lenye namba za usajili T754 AEZ lililokuwa likitoke Hedaru wilayani Same kuja Moshi imetokea LEO majira ya saa mbili na nusu asubuhi.
Kutokana na ajali hiyo magari yaliyokuwa yakielekea jijini Dar es salaa na Moshi yamelazimika kusimama na kusababisha foleni kubwa kwa muda wa masaa manne .
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mawenzi na KCMC na kwamba aliyefariki ni fundi mitambo wa lori ambapo jina lake bado halijafahamika.
Kamanda Ng’hoboko alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa Lori ambalo lilikuwa limebeba mitambo ya kutengenezea barabara na kwamba uchunguzi unaendelea na pindi utakapokamilika sheria itachukua mkondo wake.
HABARI ZAIDI NA
http://www.mazimu11.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment