Nafasi Ya Matangazo

March 03, 2010

Kero ya maji vijinini bado ni tatizo sugu.
Machi nane ya kila mwaka ni siku ya Mwanamke duniani, siku hii wanawake huitumia kujadili haki zao za msingi mbalimbali katika jamii. Hata Umoja wa Mataifa umekutana kujadili masuala mbalimbali ya wanawake katika mkutano wake wa 54 ambao pamoja na mambo mengine unajadili maazimio ya mkutano wa Beijing.

Lakini hilo likiendelea wanawake wengi vijijini wameendelea kuteseka kwa kutembea umbali mrefu na kupata shida ya kupata maji safi na salama kwaajili ya matumizi ya familia zao.

Tatizo la maji vijijini bado limekuwa sugu na kuwafanya maelfu ya akina mama waishio vijijini kutumia muda mrefu kutafuta maji kwaajili ya matumizi ya familia zao. Pichani ni wanawake wa kijiji cha Mabungo Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, wakisubiri kuchota maji katika bomba lililopo kijijini hapo.
Posted by MROKI On Wednesday, March 03, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Kwa nini watu wanafikiri hii ni kazi ya wanamama tu???

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo