Mhazini wa WAKFU ya Maendeleo ya Afrika(African Reflection Foundation-ARF) Godluck Ole Medeye(pichani) ametangaza rasmi niayake ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumteua kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Magharibi lililopo Mkoani Arusha, katika Uchaguzi Mkuu utakao fanyika baadae mwaka huu.Ole Medeye ambaye ni Kada wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, amesema amefikia uamuzi huobaada ya kufuatwa na wazee wa Arumeru magharibu wa Kada mbalimbali (vyama na kabila) kumuomba agombee Ubunge 2010.
"wazee walisema wanakero nyingi jimboni, na japo sitaweza kuzimaliza zote lakini wakasema wanaimani nitasaidiana nao vyema kuzipunguza kero hizo ambazo zimedumu kwa muda mrefu," Ole Medeye alisema.
Amesema miongoni mwa kero nyingi ambazo zinawakabili wakazi wa Arumeru Magharibi ni pamoja na Barabara mbovu (miundombinu, Maji, Huduma za Afya, Elimu ambapo kuna sekondari moja tu, pamoja na tatizo la ajira kwa vijana.
Anasema ameamua kujitolea kufanya kazi hiyo ya jamii kwani kwa imani yake anaona sasa wakati wa kuitumikia jamii yake kikamilifu umefika na kwamoyo wa dhati na wakijamaa.
Aliongeza kusema kuwa 'UBUNGE SI AJIRA NI DHABIHU" hivyo anajitolea na kama kunauwezekano Mbunge awe kama diwani apate posho tu ya kuhudhuria vikao na si kulipwa Mshahara.
Ole Medeye aliyasema hayo jana katika ofisi ya makamu Mwenyekiti wa Afrika Reflection Foundation, Upanga Dar es Salaam.






0 comments:
Post a Comment