Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2010

Mabondia wa Klabu ya ngumi ya Ashanti ya Ilala Dar es Salaam jana wakifanya mazoezi ya tumbo kwa ajiri ya mpambano wao na klabu nyingine leo.
Mabondia wa klabu ya ngumi ya Simba wakijifua kwa ajiri ya mpambano wao na Ashanti kesho.

KLABU mpya ya Mchezo wa Ngumi ya Ashanti inatarajiwa kutambulishwa kwa klabu zingine za mchezo huo Ijumaa katika ukumbi wa CCM Ilala Boma Dar es Salaam.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema Dar es Salaam jana kuwa klabu hiyo yenye mabondia 9 itatambulishwa kwa klabu zingine itambulike kuwa ni miongoni mwa klabu zinazoendeleza mchezo wa ngumi Tanzania.

Alisema utambulisho huo utakuwa chini ya taasisi ya Kinyogoli Foundation inayosiomamia kwa karibu mchezo wa ngumi Tanzania kabla ya uzinduzi wake utakaofanyika Machi mwaka huu.

Super D alisema katika hafla hiyo kutakuwa na Klabu za Simba, Vingunguti, Amana, na wenyeji Ashanti ambapo kila klabu itawakilishwa na mabondia watatu.

Alisema klabu hiyo imeanzishwa hivi karibuni na inaundwa na mabondia kama Juma Salum 'Jeshi, Yahaya Hamis, Ramadhani Ngumbo, Ramadhani Kassimu na Abdujerry Kadil.
Posted by MROKI On Friday, March 12, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo