Nafasi Ya Matangazo

March 26, 2010

Sehemu ya vifaa vya chumba cha upasuaji amabvyo vimetolewa na mradi wa Wolrd lung Foundation unaoendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Afya Ifakara na kufadhiliwa na Micheal Broomberg kutoka Marekani

Na Sara Maturo wa IHI.
Huduma ya mama na mtoto imezidi kuboreshwa kwa wakazi wa wilaya ya ulanga mkoani Morogoro,baada ya kituo cha afya Mtimbira kufanyiwa maboresho ya huduma hiyo muhimu
Kituo cha afya Mtimbira kimeanza kutoa huduma ya mama na mtoto baada ya kupata msaada wa kujenga maabara, chumba cha upasuaji, na wodi ya mama na mtoto.

Msaada wa ujenzi huo na maboresho umetolewa chini ya mradi wa World Lung Foundation unaoendeshwa na Tasisi ya utafiti wa afya Ifakara na kufadhiliwa na taasisi ya Micheal Bloomberg kutoka Marekani.

Huduma hiyo imezinduliwa rasmi 22 Machi na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dr. Rajab Rutengwe, alisema “Tumepokea msaada huu kwa mikono miwili, na ni faraja kwetu,tutauenzi na kuhakikisha unakuwa endelevu” Ni historia katika wilaya yetu, kwani tumeweza kupata msaada huu katika vituo viwili, kituo cha mwaya na hiki cha mtimbira. Alisema Dr.Rajab.

Akiongea kwa niaba ya Taasisi ya Utafiti wa Afya Ifakara, Dr. Nyamtema alisema lengo la mradi huu ni kupunguza na kumaliza kabisa vifo vya mama na mtoto “Tumeamua kuajiri mtaalam wa nusu kaputi ili kuhakikisha huduma hii inatolewa kwa mafanikio makubwa” ni imani yetu kwamba huduma hii itakuwa ya kudumu. Alisema Dr. Nyamtema

Naye Mganga Mfawithi Dr. Eliazari Kweka alisema tumefarijika kupata huduma hii ya mama na mtoto katika Wilaya yetu. “Tunaiomba Serikali ituongezee bajeti na watumishi ili kuweza kukidhi haja ya mama na mtoto” alisema Dr.Kweka
Aidha mkuu wa wilaya alisema, changamoto zinazowakabili ni kuhakikisha hakuna watoto wanaozaa watoto wenzao na kutoa huduma iliyo bora kwa mama na mtoto.

Mapema mwezi huu kituo kingine cha Afya cha Mwaya kilifanyiwa marekebisho kama hayo na kuanza kutoa huduma za upasuaji.
Posted by MROKI On Friday, March 26, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo