Nafasi Ya Matangazo

March 22, 2010

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, RPC Elias Kalinga anasikitika kutanga kifo cha mama yake mzazi Bi. Adelaide Kalinga (89) aliyefariki jana Jumapili, Machi 21 2010 saa 6 mchana jijini Mwanza.
Mwili wa marehemu unataraji kusafirishwa leo kutoka Nyakato kota za Polisi National Mwanza kwenda Iringa katika kijiji cha Wanging'ombe, Kilometa 30 kutoka Iringa mjini kando ya barabara kuu ya Mbeya ambapo mazishi yanataraji kufanyika Jumatano Machi 24,2010.

Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwa mfiwa Polisi Oysterbay -Dar es Salaam ambapo ndugu na jamaa watakutana leo saa 9 jioni, Nyakato Mwanza na Kijijini kwa marehemu Wanging'ombe Iringa.

Habari hizi ziwafikie ndugu jamaa na marafiki wa Elias Kalinga popote pale walipo.
Marehemu ameacha watoto 5, Wajukuu 25, na vilembwe 3, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jaina la Yesu lihimidiwe.
Blogu ya Watu inatoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huo.
Posted by MROKI On Monday, March 22, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo