
Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Jamii (CCJ) Richard Kiabo (kulia) ana Katibu wake Renatusi Muabi wakifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya Uzinduzi wa chama leo.

Katibu wa Muda Renatus KMuabi akionesha moja ya kadi za wana CUF ambazo wanachamawake wamezirudisha na kujiunga na CCJ leo.

Chama hichi kinaundwa na vijana ambao CCJ inasema ndio vigogo wa nchiihii, na pichani ni vigogo hao wakiwa katika uzinduzi huo.

Burudani ilikuwa ya ainayake.

Vigogo wa Chama hicho wakicheza kwa furaha, Mwenyekiti alisema chama hicho kitawawezesha kila mwananchi kula nyama tofauti na sasa ambapo nyama huliwa na wachache na waliosalia kuliwa kwa kuvizia misiba au sherehe.
Mbali na uzinduzi huo pia leo kilitarajiwa kutangaza orodha ya vigogo waliojiunga na chama hicho na badala yake wamesema vigogo waliokuwa wakizungumzia ni wananchi au jamii kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment