
Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi na Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah.

Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Elihuruma Ngowi (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Herman Mwansoko wakati wa hafla ya uzinduzi wa semina ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali leo. Wengine kutoka kushoto ni Mshauri wa Miss Tanzania Dk Ramesh Shah na Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.

Baadhi ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika semina yao katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Jackson Kalikumtima wakala wa Miss Ilala, Ben Kisaka wakala wa Miss Temeke na Asmah Makau mwandaaji wa Miss Tanga.

Baadhi ya mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwa katika semina yao katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Awetu Salim, wakala wa Wilaya ya Bagamoyo, Nasib Mahinya wakala Mkoa wa Pwani na Sylivia Mwakilufi wa Miss Njombe.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari na Utamaduni, Herman Mwansoko (kulia kwake) katika picha ya pamoja na mawakala wa Vodacom Miss Tanzania 2010 kutoka sehemu mbalimbali nchini mara baada ya hafla ya ufunguzi wa semina ya mawakala hao katika Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam.
Ndugu yangu Mahinya, 'Young Millionaire,'' uko juu.
ReplyDelete