Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia taifa wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi,Tabora leo mchana.Msanii Vicky Kamata akiwaongoza wanafunzi wa shule ya Sekoindari ya Wasichana Tabora kuimba wimbo maalumu wa Siku ya Wanawake Duniani wakati wa maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi Tabora leo mchana.
Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari mkoani Tabora wakipita na mabango mbele ya Rais Jakaya Kikwete na vioingozi wengine wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake iloiyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari mkoani Tabora wakipita na mabango mbele ya Rais Jakaya Kikwete na vioingozi wengine wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake iloiyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na vikundi mbalimbali vya wanawake wa mkoa wa Tabora wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora leo.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Tabora na mikoa mingine ya jirani waliohudhuria kilele cha sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora leo mchana.
Posted by MROKI On Monday, March 08, 2010 2 comments

2 comments:

  1. Inafurahisha kuona hii siku inakumbuka vizuri. Hongera sana akina mama wote wa Dunia hii.

    ReplyDelete
  2. Sasa huyo Viki Kamata alienda mpaka huko Tabora kote huko kwani ina maana huko Tabora hakuna Wasanii wangalioweza kuimba nakufanikisha hiyo sherehe?

    Kulikuwa kuna ulazima gani wa VIKI kutoka Dar mpaka huko tabora?

    Nisaidieni Wadau

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo