Nafasi Ya Matangazo

March 21, 2010

Maandalizi kwa ajili ya Bonanza la Kila jumapili yamekamilika katika Uwanja wa Magereza Ukonga, Ambapo Timu mbalimbali za Maveterani jijini Dar es Salaam zimepewa taarifa hiyo na kutakiwa kuwa tayari pindi wakiitajiwa kuwa tayari kwenda kushiriki ambapo michezo itakayochezwa ni mpira wa miguu na jumla ya timu sita zitakuwa zikishiriki na kila wiki timu zitabadilika kutokana na mpangilio wa ratiba.

aidha zawadi mbali zimeandaliwa kwa ajili ya timu zitakazoshinda hatua ya fainali ambapo kwa upande wa soka zawadi kwa mshindi wa kwanza ni Mbuzi, wa pili Creti Moja la Bia, na Upande wa Pool zawadi ni vivyo hivyo ambapo mshindi wa pili watapatiwa Catton moja moja ya Kinywaji cha Henken, na timu zote katika Bonanza hilo zitapatiwa kinywaji kreti moja la Bia,

zawadi zingine ni kwa mfungaji wa jumla wa mashindano(Shinigadi),Mchezaji Bora wa Mashindano(Soksi),timu itakayoshinda katika zoezi la kuvuta kamba itazawadiwa Crteti moja la Bia.

Ikumbukwe kwamba Burudani kubwa itatolewa kutoka kwa Bendi Mpya kabisa na ya kisasa ya MASHUJAA MUSICA- chini ya wanamuziki wake wote wakiwemo Zidane(Sauti ya Nyati), Ngosha Mwanamasanja(Mzee wa kuchinja Bata),Jado Fidifosi, Masoud, Raja Rada, Ibrahim Milinda Nyeusi, ambapo wapiga Gitaa Mtaalam Baba Isaya, Amosi Mkono wa Nabii, na Kiongozi nguli, nyota, katika Ulimwengu wa Muziki- Elyston Angai ambaye ndiye hatakayekuwa kiongozi kuhakikisha kwamba mambo yote yanakwenda vyema.

michezo yote itaanza majira ya saa tatu asubuhi na zichecheza kwa mtindo wa makundi ambapo kutakuwa na timu za kundi A -na B zikiwa katika makundi mawili ambapo zitacheza kwa dakika 15 mapumziko na kisha kumalizia 15 za mwisho, Chini ya Udhamini Mnono wa Kampuni ya Usafirishaji Abiria jijini Darv es Salaam ya Mamaa Sakina, na Kamnpuni ya Mashujaa Investment Group iliyoko chini ya wakurugenzi mbalimbali ikiwamo- Papaa Yohana, Papaa Tumaini, Papaa Mwololo,Papaa Maisha.

aidha timu yeyote itakayopenda kushiriki hata kama aijapelekewa barua ya kuitaarifu imetakiwa kuwasiliana na wahusika kwa namba 0658201120,0712013093 ambapo watapata maelekezo juu ya ushirikishwaji wa Bonanza Kinywaji kwa wale watakaofika kipo kwa wingi kikiambatana na nyama choma itakayokuwa ikipatikana kila juma.

kiingilio kwa wanaume ni 2000 na wanawake -Ledies FREE.

Wote mnakaribishwa kufika kila jumapili katika Uwanja wa Ukonga Magereza
Posted by MROKI On Sunday, March 21, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo