Nafasi Ya Matangazo

February 01, 2010

Mwandishi wa habari za Uchunguzi wa Kituo cha Televisheni cha TBC1 Jerry Muro ameahidi kuendeleza mapambano zaidi ya Rushwa hasa kwa jeshi la Polisi licha ya tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza kwa njia ya simu na Kituo cha Redio cha Wapo FM, Muro amesema anayo mengi yanalolihusu Jeshi hilo na sasa wameuchokoza moto atazidi kuyapakua.

"Nasema kwa hili wameuchokoza moto...ninayo mengi ambayo nimesha yafanyia kazi juu ya Jeshi la Polisi nitaendeleza mapambano dhidi ya uovu wote" alilonga Muro.

Muro mapema jana alikamatwa na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa jana jioni, juu ya tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya Shilingi Milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo.
Posted by MROKI On Monday, February 01, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo