Nafasi Ya Matangazo

February 01, 2010

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Alhaji Suleiman Kova amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo kuwa Polisi Kanda ya Dar es Salaam hawana tatizo lolote la Jarry Muro ambaye walimshikilia kwa mahijiano jana.
“Muro tulimshikilia kwa moahijiano tu kufuatia taarifa tulizopata kutoka kwa mwananchi kuwa anasumbuliwa na matapeli wanaomtisha awape rushwa ya shilingi milioni 10,” alipasha Alhaji Kova.


Alhaji Kova yaliyotokea jana ni uvumi tu kuwa Jeshi la Polisi linachuki binafsi na Mwandhsi huyo anae chipukia kuwa hatari kwa walarushwa nchini hasa Polisi usalama barabarani.
Aidha amesema Mwananchi aliyefikisha malalamiko hayo ni
Aliyekuwa Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo, Michael Wage ambaye Waziri Mkuu alimfukuza kazi kutokana na kufuja fedha za Halmashauri hiyo.

“Jamaa alifika (Wage) hapa Central Polisi juzi majira ya asubuhi saa tano na kusema kwamba kuna watu wanamsumbua na kujifanya wao ni maofisa wa polisi,PCCB, waandishi na wanajeshi wakimtisha kuwa awape fedha milioni 10,” Aliongeza Kova.

Amesema usumbufu huo ni wa muda mrefu tangu Januari 28 na walifika hata nyumbani kwake wakimtuhumu kuwa ni fisadi na anamiliki majumba na mali mkoani Morogoro.

Alhaji Kova amesema mwananchi huyo amelalamika zaidi kwamba watu hao waliokuwa na pingu wamekuwa wakimwambia kwamba asipotoa fedha hizo watamchukulia hatua kali za kisheria.
Alisema baada ya kufika katika eneo hilo lengo likiwa ni kuwakamata matapeli hao, gari lenye namba T 545 BEH aina ya Toyota Cresta liliingia lakini mwenyewe alikataa kushuka na kumtaka Wage kufuata gari hilo.

“Polisi wangu walipoona gari limekuja na watuhumiwa kukataa kushuka walilifuata na walipofika walishangaa kumuona ni Jerry Muro na baada ya Wage kusema huyu ndiye ambaye amekuwa akinisumbua sana polisi ilibidi wamchukue mpaka kituo cha polisi ili kupata maelezo mazuri” alisema.

Kova alisema mlalamikaji huyo alikuwa akidai kwamba anamfahamu Jerry na amekuwa akimsumbua sana mpaka akamfuata nyumbani kwake na kukubaliana wakutane mjini Januari 29 na kutoa vithibitisho mbalimbali kwam,ba anamfahamu ikiwermo miwani yake aliyokuwa ameiacha katika gari lake.

Silaha ya Muro inamilikiwa kihalali ambayo ni bastola CZ97B namba A6466 na kwa upande wa kumiliki pingu Kova alisema ni kinyume cha sheria kutokana na kwamba pingu humilikiwa na polisi au magereza pekee.

Kamanda huyo ambaye anapenda sana kuzungumza na vyombo vya habari pindi liyokeapo tukio alisema kuwa jeshi hilo limemtaka Muro kuwasilisha risiti ya pingu hiyo kutokana na kwamba hakuna sehemu yoyote inapouzwa na sheria haimruhusu mtu yeyote kumiliki labda makampuni na ni kwa kibali maalum.

Hata hivyo Kova alisema kuwa kesi hiyo haitaenda mahakamani mpaka ipitie kwa wakili wa serikali na kueleza kwamba Jerry yupo nje kwa dhamana na kuwataka watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wajisalimishe.
Posted by MROKI On Monday, February 01, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo